Mfumo wa maombi umefungwa kwasababu muda wa kupokea maombi ya kujiunga na shule umekwisha. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Tafadhali usifanye malipo na ikiwa umefanya malipo rudisha muamala.
Jinsi ya kujiunga na shule yetu
Maelekezo ya kununua fomu mtandaoni
Lipia TSh 25,000/= kwenye namba ifuatayo
0685 010 334 Jina: JOHN MNUNGA
Tumia namba ya simu kufanya malipo. Usiweke pesa kwa wakala wala kuhamisha toka benki. Ukitumia wakala / benki hatutapata namba ya simu iliyofanya malipo hivyo mifumo yetu haitaweza kushughulikia muamala wako
Ndani ya muda mfupi tutakutumia ujumbe kwenye namba uliyoitumia kufanya malipo. Ujumbe huo utakuwa na token.
Bonyeza Pakua fomu. Ingiza namba ya simu uliyotumia kufanya malipo.
Ingiza token tuliyokutumia kwa ujumbe mfupi
Ingiza majina mawili ya mwanafunzi kwenye sehemu husika
Hakiki jina la mwanafunzi. Hutaweza kubadilisha baada ya hatua hii.
Kama ni sawa bonyeza Hifadhi Taarifa